Picha za wasifu zinazoruhusiwa

Ukisoma maelezo haya, kuna uwezekano utagundua picha uliyopakia inaenda kinyume na kanuni zetu za matumizi ya mtandao huu. Hapa chini tumeorodhesha baadhi ya sababu zinazotufanya tufute picha zako.

1. Ni mtu maarufu

Ikiwa unapakia picha ya mtu mwingine, hiyo ni kinyume cha kanuni zetu. Hakuna ubaya ikiwa picha yako umekaa na marafiki na jamaa, lakini kama ni Barack Obama au Lionel Messi, hatuwezi kuamini kwamba ni wewe. Kama umeshikana mikono na mmoja wao, basi ni sawa lakini picha ya wasifu inabidi iwe ile ambayo wewe mwenyewe unaonekana.

2. Ni mtoto

…na inawezekana ni mtoto mrembo kweli kweli! Na ni muhimu kumjuza mwenza mtarajiwa kwamba una mtoto, lakini picha ya kwanza kwenye wasifu lazima iwe ni yako mwenyewe, na picha ya pili na zingine zinaweza kuwa za mtoto kwenye albamu.

3. Ni skrinishoti ya Instagram

Picha ambazo ni skrinishoti zinaenda kinyume na kanuni zetu. Kama ni picha yako mwenyewe, basi tuna imani unayo picha asili kwenye simu yako. Tumia picha hiyo asili kuipakia kwenye wasifu wako na sio skrinishoti.

4. Ni nukuu mzuri

Na inawezekana tumejifunza jambo kutoka kwenye nukuu husika, lakini ni muhimu kwenye picha ya kwanza unakuwa wewe mwenyewe. Ukweli ni kwamba, nukuu inaweza kuwa jambo bora sana linaloweza kusaidia kutoa taswira ya wewe ni mtu wa aina gani hasa. Hata hivyo, picha ya kwanza ya wasifu ni lazima iwe ya kwako mwenyewe na hii nukuu unaweza kuiweka kwenye albamu ya wasifu wako.

5. Inaweza kuonekana kama tangazo la biashara

Hiyo ni sababu tosha kabisa ya kufuta picha husika. Hatupendi kutangaza kitu ambacho hatujaidhinisha, hivyo basi, kama unataka kutangaza, wasiliana nasi kwanza.


Unataka mafanikio zaidi kwenye mtandao huu?

Tafadhali pitia makala hii kuhusu ni namna gani unaweza unaweza kuboresha wasifu wako na kuwa bora zaidi kuwazidi wengine.