Matakwa na masharti

Tunapenda watu wajisikie salama wanapotumia tovuti yetu. Kutokana na hilo, tumetengeneza sheria na viwango vya kijami vinavyoendana na maadili yetu, kama ilivyoahinishwa hapa chini.

Sheria hizi zimewekwa ili kukupatia huduma bora na salama kadri iwezekanavyo.

 

Sheria kwenye Dating.co.tz

Usipotii au kufuata sheria zetu, tunaweza kufuta akaunti yako, na taarifa zako bila kukuarifu. Tuna haki kurekebisha au kuifuta akaunti yako muda wowote bila kukupa taarifa endapo utakiuka sheria zetu na viwango vya kijamii tulivyoweka.

Ili kufungua akaunti kwenye tovuti ya dating.co.tz, unatakiwa kuwa na umri wa angalau miaka 18.

Unapaswa kutoa barua pepe iliyo sahihi ambayo pia ni ya kwako mwenyewe. Ni kosa kisheria kutumia barua pepe bandia, au kutumia barua pepe ya mtu mwingine.

Kwa kutoa barua pepe yako, unakubali kwamba tunaweza kukutumia taarifa, ushauri na makala zinazohusiana na mtandao wa dating.co.tz.

Huruhusiwi kutangaza bidhaa na huduma bila ruhusu yetu.

Huruhusiwi kutuma kwa watumiaji wengine maudhui yenye matangazo ya biashara na huduma, maudhui ya kukera na maudhui yenye ubaguzi.

Huruhusiwi kuwakera wengine, kufanya mambo yasiyofaa kwa wengine na kufanya ubaguzi wa aina yoyote.

Mawasiliano yanayoashiria kutaka ngono na watoto wadogo, au maudhui yoyote yaliyo kinyume na sheria yataripotiwa polisi bila kutoa tahadhali. Barua pepe na anuani ya utambuzi ya intaneti, yaani IP Adress, na taarifa zingine zozote zinazoweza kufanikisha utambuzi wako, zitawasilishwa polisi.

Picha ya wasifu inatakiwa kuwa ya kwako mwenyewe, na sio ya mtu mwingine. Inapaswa kuwa ya siku za karibuni, na una hatimiliki nayo.

Picha haipaswi kuwa na nembo, kiunganishi cha intaneti; yaani links, namba za simu au taarifa zinazoelekeza kwenda kwenye tovuti zingine.

Picha hazitaashiria vurugu au kutisha, au namna yoyote inayoashiria matendo yaliyo kinyume na sheria.

Picha ya wasifu na zile za kwenye albamu hazipaswi kuwa za utupu. Matiti na sehemu za siri zinapaswa kufunikwa. Picha za namna hiyo zinaruhusiwa kubadilishana kwa meseji za siri pekee, yaani DM.

Picha zitakazoonekana kuwa ni za wanamitindo, watu maarufu, wanasiasa, wachezaji wa soka, wanamuziki au za kugushi, zitaondolewa mara moja bila ya kutoa tahadhali.

Hitaji lolote kutoka kwa msaidizi wa tovuti linapaswa kufuatwa. Ni muhimu kufanyia kazi onyo au ushauri. Endapo onyo litapuuzwa, akaunti yako itafutwa.

Wakati wowote, na tena bila hata ya taarifa, tunaweza kufuta ujumbe au wasifu ikiwa kanuni yoyote iliyotajwa hapo juu, itakiukwa. Hautarudishiwa pesa zako ikiwa utashindwa kufuata sheria tajwa hapo juu.

Tunaondoa maudhui, kufuta akaunti, na kufanya kazi na vyombo vya dola endapo tunaamini kuna hatari ya kutokea madhara ya kimwili au vitisho vya moja kwa moja kwa usalama au faragha ya mtumiaji yeyote wa tovuti hii.

 

Faragha

Tovuti ya dating.co.tz inawajibika chini ya sheria mbalimbali zinazohusu matumizi na usalama wa taarifa binafsi za watumiaji wake, na inawajibika kulinda haki ya usiri wa watu. Inapotokea udhalilishaji wa aina yoyote, au matendo yoyote yanayokiuka sheria yakitokea kwenye tovuti hii, polisi wataarifiwa, na taarifa zote muhimu, ikiwa ni pamoja barua pepe na anuani ya intaneti, vitatolewa kwa mamlaka husika.

Hatutoi taarifa zako kwa wasiohusika na tovuti hii.

Tunashea jina unalotumia hapa, jinsia yako, umri, picha ulizopakia, mkoa na mji unaoishi kwa wanajamii wengine waliopo kwenye mtandao huu, lakini katu hatutashea taarifa hizo kwa wasio wanajamii wa mtandao huu.

Hatutoi barua pepe yako, nywila na taarifa zingine za siri bila ridhaa yako. Faragha na usalama wako tunavichukulia kwa umakini wa hali ya juu, na kwahiyo nywila yako inahifadhiwa kwenye mfumo ambao si rahisi kufikiwa na mwanadamu yeyote.

Endapo unataka akaunti na taarifa zako zote zifutwe, unaweza kufanya hivyo wewe mwenyewe baada ya kuwa umeshaingia ndani, yaani baada ya ku-login. Ukishafuta akaunti yako, itakuwa umefuta taarifa zako zote moja kwa moja. Taarifa hizo zikiwa ni pamoja na picha, ujumbe uliotuma na kutumiwa na data zingine. Tunahifadhi taarifa zote za tovuti kwa siku 30. Baada ya siku 30, taarifa zote zitafutwa moja kwa moja.

Endapo miaka 3 itapita bila akaunti yako kutumika, moja kwa moja itafutwa. Hata hivyo, kabla ya kufutwa, utapewa taarifa.

Tunafuatilia matumizi ya mtandao kwa kila mtumiaji na tabia zake. Lengo la kufanya hivi ni kuchambua matumizi ya mtandao kwa lengo la kufanya maboresho ili mtumiaji apate kile kilicho bora zaidi.

 

Kwa usalama wako

Kuwa mwangalifu unapotoa namba yako ya simu, jina unalotumia WhatsApp, au anuani kwa mtu mwingine. Tunashauri usifanye hivyo hadi unahakikisha hauna mashaka na mtu unayechati nae. Ili mradi unachati nae kupitia mtandao wetu, basi muda wowote unaweza kumzuia, yaani kumbloku usiyemtaka.

Usitoe taarifa zako za kibenki. Hakuna sehemu yoyote kwenye tovuti ya dating.co.tz tunapokutaka ufanye malipo isipokuwa kupitia kituo cha malipo.

Dating.co.tz inakushauri kukutoa pesa kwa mtu yeyote usiyemfahamu au ambae hujakutana nae hata kama umebadilishana nae namba ya simu na kuchati nae mara kadhaa. Fahamu kwamba, ombi lolote la pesa linalenga kukutapeli pesa zako, na kamwe hutarudishiwa.

Uanachama wako hapa ni wa kwako binafsi, na usitumiwe na mtu mwingine yeyote.

Dating.co.tz haitawajibika juu ya mtumiajia yeyote asiyefuta sheria zilizotajwa hapo juu.

Kwa kutumia tovuti hii, unakubaliana na sheria na masharti ya mtandao huu.

 

Kuingia kwa kutumia mitandao ya kijamii

Unapochagua kujisajiri au kuingia kwa kutumia mtandao wowote wa kijamii au kwa kutumia huduma nyingineyo ya upande wa tatu, taarifa pekee tunayotuimia ni anwani yako ya barua pepe na kuithibitisha ili kujiridhisha kwamba ni wewe. Tunahifadhi anwani yako ya barua pepe kwa namna ile ile kama ambavyo ungejisajiri au kuingia ndani kwa kutumia barua pepe yako pasipo kutumia huduma nyingine yoyote ile. Hatutoi kwa wengine taarifa yako yoyote ile na hatuhifadhi taarifa yako yoyote kuhusu wewe, hata kama tungekuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Tunahifadhi barua pepe yako tu. Hatuchukui neno lako la siri ulilotumia kujisajiri au unalotumia kuingia ndani. na hivyo neno hilo halitafahamika kabisa na sisi. Endapo ungependelea kuingia pasipo kutumia mtandao wa kijamii au kwa kutumia huduma nyingine ya upande wa tatu basi unaweza kufanya hivyo wakati wowote. Endapo unataka kufuta data zako zote, unaweza kufanya hivyo mwenyewe kwa urahisi kabisa kwa kubofya kitufe cha Mipangilio. Unapofuta akaunti yako, taarifa zako zingine zote zinafutika kwenye jukwaa letu na hakutakuwa na huduma yoyote baada ya hapo. Barua pepe yako kamwe haitatolewa kwa mwanachama yeyote yule wa jukwaa letu au kutolewa popote pale nje ya jukwaa hili.

 

Malengo yanayotufanya tuchakate taarrifa zako

Lengo kuu la kuchakata taarifa zako kutoka kwenye mtandao wowote wa kijamii ni kukurahisishia wakati wa zoezi la kujisajili na kuingia kwenye mtandao. Kama ilivyoelezwa hapo juu, tunachohifadhi ni anwani yako ya barua pepe tu. Kuna sababu mbili zinazotufanya tuhifadhi barua pepe yako. 1. Endapo baadae unajaribu kuingia kwenye mtandao wa dating.co.tz kwa kutumia anwani yako ya barua pepe badala ya kutumia mtandao wa kijamii, itawezekana kufanya hivyo. 2. Tunaweza kukutumia barua pepe endapo umesahau nywila yako (yaani neno la siri) au kama tuna taarifa yoyote muhimu kwako au kama unaamua kupokea barua pepe za kiotomatiki kutoka kwetu kama vile majarida, wanachama wenye sifa utakazo, taarifa za ujumbe mpya, n.k.

 

Jinsi unavyoweza kuomba kufutwa kwa taarifa zako.

Kama unataka taarifa zako zote zifutwe kutoka kwenye mtandao wetu, unaweza kufanya hivyo wewe mwenyewe, tena kwa urahisi kabisa kwa kubofya kitufe kilichoandikwa Mipangilio. Utaweza kufanya hivyo baada ya kuingia kwenye mtandao. Kama unafuta akaunti yako kutoka kwenye mtandao wetu, basi kila kitu kinachokuhusu wewe kitafutika na hakutakuwa na uhusiano wowote na kwa huduma yoyote baada ya kuwa umefuta akaunti yako. Wakati wote una haki ya kusahaulika na haki ya kufuta taarifa zako. Hata hivyo, tafadhali zingatia kwamba, katika mazingira fulani, tunaweza tusikubaliane na ombi lako kutokana na sababu za kisheria. Kama inatokea hivyo, tutakutaarifu wakati unapoomba kufutwa kwa taarifa zako. Inapotokea huoni kitufe cha kufuta akaunti yako, unaweza kutuandikia kupitia support@dating.co.tz na kuomba kufutwa kwa akaunti yako, nasi tufanya hivyo kwa niaba yako.