Hejsa for den.

Jilinde mwenyewe na walinde wengine kwa corona virus

 

Virusi vya corona vipo, na tunakutaka uwe mwangalifu!

Ustawi na uzima wako ndivyo vipaumbele vikuu kwetu! Jukwaa letu ni sehemu bora kabisa katika kukukutanisha na marafiki wapya. Na ingawaje tunapenda ufurahie maisha yako hapa lakini kujikinga na virusi vya korona ni jambo muhimu sana. Hivyo basi, tunashauri njia za kujikinga na virusi vya korona zikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kubeba vitakasa mikono, kuepuka kugusa uso wako na kuhakikisha unakaa mbali na watu kwenye mijumuiko.

 

Hii ikiwa ni pamoja na kujizuia kubusiana, kukumbatiana pamoja na kushikana mikono na mpenzi wako mtarajiwa.

 

 

Ushauri kutoka Shirika la Afya Duniani, yaani WHO

(World Health Organisation) https://www.who.int/

 

Osha mikono yako mara kwa mara

Safisha mikono yako mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji safi yanayotiririka, au tumia vitakasa kusugulia viganja vyako.

Kwanini? Virusi ambavyo vinaweza kuwa mikononi mwako vitakufa endapo utaosha mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka au ikiwa utatumia vitakasa mikono kusugua viganja vyako.

 

Epuka kukaribiana na watu

Hakikisha unakaa au kusimama umbali wa angalau mita 1 (yaani futi 3) kutoka alipo mtu yeyote anayekohoa au kupiga chafya.

Kwanini? Wakati mtu anapokohoa au kupiga chafya, anakuwa anasambaza vimajimaji kupitia mdomo au pua. Kama mtu huyu ana virusi vya corona, basi vimajimaji hivi pia vitakuwa na virusi. Sasa ukikaa karibu na mtu wa aina hii, hivi vimajimaji vyenye virusi vya corona vitaingia mwilini mwako kwa njia ya pua au mdomo, na hivyo kukuambukiza.

 

Jizuie kugusa macho, pua na mdomo

Kwanini? Kama tujuavyo, mikono huwa inagusa sehemu nyingi, na ikiwa sehemu hizo zina virusi vya corona, basi mikono itabeba hivyo virusi.  Mikono hii ikishakuwa na virusi basi inaweza kusafirisha virusi hivyo vya corona hadi kwenye macho yako, mdomoni au puani. Kutokea hapo, virusi vya corona vinaweza kuingia mwilini mwako na kukusababishia ugonjwa wa virusi vya corona.

Kumbuka kwamba, virusi vya corona vinaweza kuishi hata kwenye sehemu ngumu kamavile juu ya meza, kwenye kompyuta na hata simu; simu ambazo mara kwa mara huwa tunazigusa kwa mikono yetu.

 

Jifunze kutumia njia safi na salama za kupumua

Hakikisha wewe, na walio jirani yako mnafuata njia safi na salama za utoaji hewa. Hii maana yake ni kwamba, ikiwa unapiga chafya au kukohoa, basi hakikisha unaziba mdomo au pua kwa kutumia karatasi nyepesi za tishu, au kunja mkono wako kisha ukohoe au kupiga chafya kwenye kiwiko. Ukitumia tishu, basi tishu zilizotumika zitupie sehemu maalumu mara moja.

Kwanini? Vitone au vimajimaji vinavyotokana na kukohoa au kupiga chafya huwa vinasambaza virusi. Unapotumia njia salama za utoaji hewa, itakuwa unawalinda watu wa karibu dhidi ya virusi kama vile vinavyosababisha homa, mafua na virusi vya corona, yaani COVID-19.

 

Endapo una homa, unakohoa, au unapumua kwa shida, basi fanya haraka ukaonane na wataalamu wa afya

Kama hujisikii vizuri basi tulia nyumbani. Kama una homa, kikohozi, au unapata shida wakati wa kupumua, basi fanya haraka ukaonane na mtaalamu wa afya. Fuata maelekezo ya wataalamu wa afya waliopo maeneo unayoishi.

Kwanini? Wataalamu wa afya, katika ngazi ya taifa au ya mtaa watakuwa na taarifa za karibuni kabisa kuhusiana na hali ya virusi vya corona kwenye eneo au mji unaoishi. Kama utaweza kuwapigia kabla hujaenda, itawasaidia kukuelekeza haraka ni sehemu ipi sahihi unayoweza kwenda kutokana na tatizo lako.Hii pia itakusaidia wewe binafsi na pia itasaidia kuzuia kusambaza virusi na maambukizi mengine.

 

Hakikisha unafuatilia taarifa na fuata ushauri unaotolewa na watalaamu wa afya na serikali.

Kwa maelezo zaidi ya kujikinga wewe mwenyewe na kuwakinga wengine dhidi ya virusi vya corona, unaweza kutembelea tovuti ya Shirika la Afya Duniani kwa kubofya Hapa.

Picha za wasifu zinazoruhusiwa

Ukisoma maelezo haya, kuna uwezekano utagundua picha uliyopakia inaenda kinyume na kanuni zetu za matumizi ya mtandao huu. Hapa chini tumeorodhesha baadhi ya sababu zinazotufanya tufute picha zako.

1. Ni mtu maarufu

Ikiwa unapakia picha ya mtu mwingine, hiyo ni kinyume cha kanuni zetu. Hakuna ubaya ikiwa picha yako umekaa na marafiki na jamaa, lakini kama ni Barack Obama au Lionel Messi, hatuwezi kuamini kwamba ni wewe. Kama umeshikana mikono na mmoja wao, basi ni sawa lakini picha ya wasifu inabidi iwe ile ambayo wewe mwenyewe unaonekana.

2. Ni mtoto

…na inawezekana ni mtoto mrembo kweli kweli! Na ni muhimu kumjuza mwenza mtarajiwa kwamba una mtoto, lakini picha ya kwanza kwenye wasifu lazima iwe ni yako mwenyewe, na picha ya pili na zingine zinaweza kuwa za mtoto kwenye albamu.

3. Ni skrinishoti ya Instagram

Picha ambazo ni skrinishoti zinaenda kinyume na kanuni zetu. Kama ni picha yako mwenyewe, basi tuna imani unayo picha asili kwenye simu yako. Tumia picha hiyo asili kuipakia kwenye wasifu wako na sio skrinishoti.

4. Ni nukuu mzuri

Na inawezekana tumejifunza jambo kutoka kwenye nukuu husika, lakini ni muhimu kwenye picha ya kwanza unakuwa wewe mwenyewe. Ukweli ni kwamba, nukuu inaweza kuwa jambo bora sana linaloweza kusaidia kutoa taswira ya wewe ni mtu wa aina gani hasa. Hata hivyo, picha ya kwanza ya wasifu ni lazima iwe ya kwako mwenyewe na hii nukuu unaweza kuiweka kwenye albamu ya wasifu wako.

5. Inaweza kuonekana kama tangazo la biashara

Hiyo ni sababu tosha kabisa ya kufuta picha husika. Hatupendi kutangaza kitu ambacho hatujaidhinisha, hivyo basi, kama unataka kutangaza, wasiliana nasi kwanza.


Unataka mafanikio zaidi kwenye mtandao huu?

Tafadhali pitia makala hii kuhusu ni namna gani unaweza unaweza kuboresha wasifu wako na kuwa bora zaidi kuwazidi wengine.

Jinsi ya kuufanya wasifu wako kuwa bora

Linapokuja suala la kutafuta mwenza mtandaoni, ni muhimu kujitofautisha na wengine na kuwa na wasifu uliosukwa vizuri na kuwa bora. Kwa wengine kuandika wasifu wao inaweza kuwa changamoto lakini hapa tutawaelekeza jinsi ya kukurahisishia suala hilo. Tumekuandalia vidokezo vitano vitakavyokusaidia kuufanya ukurasa wa wasifu wako kuwa bora zaidi.

1. Pakia picha mbalimbali

Wasifu wenye picha mbili au zaidi unapata Pendwa, yaani “Likes” na ujumbe mwingi zaidi kuliko wasifu wenye picha moja au usiokuwa na picha kabisa. Unapopakia picha zako, jitahidi kuchagua zile zenye muonekano tofauti tofauti. Picha hizi ni kama zile zinazokuonesha umbo lako lote, picha zinazokuonesha uso wako vizuri, au labda picha zinazokuonesha ukifanya zile shughuli uzipendazo. Watu wapo vizuri sana katika kuzing’amua picha, na tunayafanya haya ndani muda mfupi sana, tena chini ya sekunde moja!
Kumbuka kwamba mtu anayeiona picha yako hakufahamu, hivyo basi hapa ndipo pahala muafaka kwa watu kujenga taswira ya wewe ni nani hasa. Fanya hima na pakia picha yako mzuri sasa!

2. Andika vizuri maelezo ya wasifu wako

Wakati wa kuandika maelezo ya wasifu wako, kama ilivyo kwa picha zako, fikiria kwamba anayesoma wasifu huo alikuwa hakufahamu hapo kabla. Toa taswira mzima kuhusu wewe. Ingia kwa undani kuhusu mambo unayoyajali. Jizuie kueleza yale usiyoyapenda. Andika kuhusu mambo yanayokupa furaha. Je, una shauku ya jambo fulani? Inaweza kukuwea rahisi kuandika kuhusu ulichona na shauku nacho endapo huwa unapata shida ya kuandika kuhusu wewe. Fikiria kuhusu maelezo ya wasifu wako sawa na kitabu. Inabidi ianze kwa ushawishi na kuvuta hisia. Ziteke hisia za msomaji mara anapoanza kusoma wasifu wako, hususani kama unaamua kuandika maelezo marefu kuhusu. Songa mbele na jaribu sasa!

3. Chunguza makosa ya kiuandishi

Jipatie rafiki mzuri akisoma wasifu wako usio na makosa ya kiuandishi. Jambo unaloweza kufanya ni kurudia kuusoma wasifu wako baada ya kuwa umeshamailiza kuuandika. Kwa mtindo huo, utaweza kuyaona maelezo ya wasifu wako kama yatakavyoonekana na watu wengine, na hivyo kukuwezesha kuziona hitilafu za kimaandishi kwenye maelezo yako.

4. Ufanyie marekebisho wasifu wako mara kwa mara

Hakikisha wasifu wako unakuwa wa leo leo. Kwa mfano, kama ni mwezi wa Disemba basi itapendeza kweli kweli ikiwa wasifu wako utakuwa na maelezo ya kuwatakia watu Krismasi Njema lakini itakuwa ni kiroja endapo ujumbe huo wa Krismasi Njema utabaki hapo kwa muda mrefu hata baada ya siku ya Krismasi kuwa imeshapita. Ni sahihi pia kama unaandika “Umri wangu ni miaka 32, na ninaishi…” na maelezo ya wasifu wako yanabaki hivyo bila kubadilisha wakati umeshatimiza miaka 33.

5. Pakia picha mpya

Unapopakia picha mpya kwenye wasifu wako, unapata watembeleaji wengi zaidi na hivyo kukuongezea nafasi ya watu kukutumia ujumbe. Watu watajenga dhana kwamba, wasifu wako ni mpya na unaovutia.

Aidha tukujuze endapo picha za kwenye wasifu wako ni za zamani.


Umeshawahi kuona picha yako ya wasifu ikifutwa na utawala lakini hukufahamu ni kwanini?

Tafadhali pitia kanuni kuhusu picha ya wasifu, huenda ukapata jibu hapa 🙂